Mbowe amemkumbuka Gadafi na Nyerere salamu za Mwaka Mpya
Mbowe amemkumbuka Gadafi na Nyerere salamu za Mwaka Mpya
January 1, 2018 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Hai, Freeman Aikael Mbowe amemshukuru MUNGU kwa kumvusha mwaka 2017 na kuingia mwaka mpya wa 2018 na kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook wenye zaidi ya watu elfu hamsini Mbowe amekumbushia baadhi ya itikadi za aliyekuwa kiongozi wa Libya Muhamar Gadafi na Mwl. Nyerere na kusema CHADEMA itaendelea kupigania haki katika Taifa la Tanzania
Namnukuu Mbowe “CHADEMA tutaendelea kupigania haki na demokrasia katika Taifa letu, 2018 kamwe hatutaogopa vitisho, kamatakamata ya viongozi wa Upinzani kama tulivyoshuhudia 2017, tutaendelea kupigania utawala unaofuata sheria,” – Freeman Mbowe
No comments: